Mafunzo
Kutokana
na kuanza kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano
hapa Tanzania na Mafunzo mbalimbali yanayotolewa katika
taaluma ya Kompyuta bado hakuna mafunzo rasmi yanayoelekeza
kupatikana kwa wataalam katika sanaa ya kompyuta pia utayarishaji
filamu na vipindi mbalimbali vya televisheni hapa nchini.
Kampuni yetu imedhamiria kuwekeza katika taasisi ya mafunzo
yenye kiwango cha kimataifa ili kutoa mchango katika sekta
ya utayarishaji filamu ambayo kwa siku za hivi karibuni
imeanza kupata mwelekeo mpya hivyo kuwepo kwetu kutaleta
thamani zaidi na kuingiza kazi zilizotayarishwa Tanzania
katika soko la kimataifa na hivyo kuipatia nchi fedha za
kigeni na kuitangaza katika anga za kimataifa. Kwa jinsi
hii kizazi cha wasanii, watayarishaji filamu na wadau wengine
watapata matumaini mapya ya siku za usoni. Taasisi
yetu ya mafunzo itazingatia uwezo wa mwanafunzi kitaaluma
na hivyo kuwapokea hata wale wenye uwezo mdogo wa fedha
lakini wenye vipaji na uwezo wa kufuata mafunzo. Tuna amini
ya kwamba vijana wa Tanzania ni hodari na wanaopenda kujifunza
wakipewa fursa na dira sahihi.