Ajira

Tunazo nafasi za kazi katika maeneo ya miradi ya 3D-computer animations pia inahusisha kufundisha wafanyakazi. Ingawaje uwezo wetu wa kifedha katu haulingani na ule wa makampuni ya Ulaya na Amerika, bado tuna amini ya kwamba tunaweza kutoa vivutio vingine tofauti kwa wataalam wageni. Ofisi zetu ziko hatua chache tu kutoka pwani ya bahari ya hindi na karibuni kama kilomita 40 kutoka visiwa vya Unguja na Pemba ( Zanzibar ) hivyo tunafanya kazi katika maeneo ambayo watu wengine hufunga safari kwenda mapumzikoni! Iwapo wewe ni mtu uwezaye kufanya kazi miongoni mwa wengine na una taaluma,ujuzi na uzoefu kama graphic artist na ungependa kufundisha wengine wapate ujuzi kama wako hasa wanafunzi wetu wa Kitanzania, tafadhali tuma maombi yako kwa:, ukifaulu tutakuwezesha kupanda ndege haraka iwezekanavyo uje Tanzania kujiunga nasi!

Sifa

  1. Shahada ya Chuo kikuu katika nyanja ya Graphics na uelewa katika 3D Max au Maya Photoshop. Utafikiriwa zaidi kama una ufahamu mzuri wa Autodidacts.
  2. Atakaye faulu ata funga mkataba wa miaka isiyopungua 2(Iwapo utajilipia gharama ya Viza na usafiri, pia uwezekano wa mkataba wa mwaka 1 waweza kujadiliwa)
  3. Ufasaha katika kuongea na kuandika lugha ya Kiingereza ni sifa ya lazima Ufahamu wa lugha ya Kiswahili na Kijerumani ni sifa ya ziada.