Kampuni

Keystone Animation Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa na mwana historia na mtayarishaji filamu wa Kijerumani aitwaye Christoph Neubauer akishirikiana na mtanzania jijini Dar-es-salaam – Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Muasisi huyu anatumaini kwamba kuanzishwa na kufanya kazi kwa mafanikio kwa kampuni hii kutavutia wawekezaji wengi zaidi kutoka nje kuja kuwekeza katika nyanja ya teknolojia ya sanaa ya kompyuta (computer graphics and animations) pia fani ya utayarishaji na utengenezaji filamu.

Mtazamo
Mtazamo wetu umejikita katika utayarishaji wa filamu za mafunzo (documentaries) Kutokana na mada mbalimbali za kihistoria zilizo fanyiwa utafiti wa kina kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya sanaa ya 3D computer animations. Ujenzi mpya wa sanifu za kihistoria zilizotoweka kutokana na ukale wake ndio mhimili mkuu wa kazi yetu. Yote haya yanafanyika huku tukizingatia umuhimu na usahihi wa historia.

Ubora na Viwango
Ili kuhakikisha ubora na viwango vinafikiwa katika filamu tunazotayarisha, kampuni hutumia huduma za utengenezaji au uchapishaji kutoka kampuni mwenza ijulikanayo kama "Christoph Neubauer publishing" iliyoko Ujerumani, na ni kwa jinsi hii tu tunaweza kufikia ufanisi wa juu katika ubora na viwango vitakiwavyo kimataifa.

Changamoto nchini Tanzania
Kwa vile lengo letu kubwa ni kujikita katika utayarishaji na utengenezaji wa filamu za kimafunzo na hasa zile zenye mwelekeo wa kihistoria na kuziweka katika mfumo wa DVD tayari kwa mauzo, katika soko la kimataifa, zipo changamoto kadhaa zinazo jitokeza hapa nchini Tanzania. Tanzania , ikiwa nchi mojawapo katika mataifa yanayoendelea ya ulimwengu wa tatu Utafiti unaonyesha kwamba, ni asilimia kumi tu (10%) ya watu wote wenye kufikiwa na huduma ya umeme, ambapo sehemu kubwa wapo mijini na ni asilimia mbili tu (2%) ya watu wenye kupata huduma ya teknolojia ya habari kupitia mtandao wa kompyuta (Internet) Hali hii inaleta changamoto kubwa hasa kwa kampuni ambayo shughuli zake zinategemea zaidi umeme wa uhakika, teknolojia ya kompyuta, habari na mawasiliano Yenye kuwepo wakati wote.Changamoto nyingine inatokana na upungufu au ukosefu wa wataalam waliofuzu vizuri Katika nyanja za taaluma ya sanaa ya kompyuta (computer graphics and animation) na utayarishaji na utengenezaji wa filamu. Ili kukabiliana na changamoto hii, kampuni inadhamiria kuwekeza katika kutoa mafunzo mbalimbali ya kitaaluma ili kujenga uwezo wa rasilimali watu nchini Tanzania. Kama ilivyo kwa nchi nyingi zinazoendelea, Tanzania nayo haijajiunga na taratibu za Kimataifa zinazo ratibu nambari maalumu za bidhaa katika biashara. (Global Trade Item Number) ambazo huwezesha uingizaji wa bidhaa katika soko la kimataifa. Kutokana na changamoto hii mauzo ya filamu zitokazo nchini kwenda kwenye soko pana duniani, hayatawezekana kwa kuwa vigezo hivyo muhimu vinapaswa kuzingatiwa kwanza.Kwa sababu hii kampuni ya Keystone Animation Ltd kupitia kampuni dada iliyoko Ujerumani ita chapisha na kuratibu kazi zote na kuziingiza katika soko la kimataifa Kwa urahisi na faida.