Filamu hapa nchini

Kama zilivyo nchi nyingi katika bara la Afrika ambapo utayarishaji na utengenezaji wa filamu za ndani haujapata mwamko mkubwa, hapa Tanzania hali si tofauti tumeshuhudia filamu nyingi zinazohusu habari za ndani ya nchi zikitengenezwa na watu wa nje, ambapo mara nyingine zimeibua mijadala na misuguano kutokana na kukinzana na masuala muhimu ya ukweli ,maadili na uhalisi wa mada. Tungependa kushiriki katika uibuaji, utayarishaji na utengenezaji wa filamu za Kitanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na hasa wanahabari , waongozaji, na watayarishaji wa filamu ambapo tutapokea tahariri zao kisha kuchambua mada itakayokua na maudhui, ujumbe au mawazo yanayokubalika na kisha kushiriki katika uzalishaji wake kwa viwango na ubora wa kimataifa ili kukuza na kutangaza jina la Tanzania na mtengenezaji wa filamu husika,tutaipeleka kwenye vituo vya televisheni mbalimbali duniani ili ipate kuonyeshwa na kuwa tumesaidia kuitangaza. Pia filamu hiyo itawekwa kwenye tovuti yetu ambapo itatangazwa duniani wakati wote.

Keystone Animation Ltd inajivunia mafanikio iliyofikia baada ya kuwa imetayarisha na kuingiza sokoni filamu zake zinazohusu historia ya mji wa Berlin huko Ujerumani ambazo zimepokelewa vema na kupata mauzo ulaya na Marekani. Ni kwa uzoefu huu tungependa kuandaa filamu au vipindi mbalimbali vya televisheni kuuelezea ulimwengu juu ya mafanikio ya Afrika na changamoto zilizopo kufikia malengo ya millennia.